Posts

Je, Ushuhuda Wako Unajenga au Unaua Imani ya Wengine?

Image
SOMO: Jinsi Shuhuda Zinavyokuza au Kudumaza Imani ya Mkristo? Bwana Yesu asifiwe sana, mtu wa Mungu.  Namshukuru sana Mungu kwa kunipa kibali cha kukutana nawe tena, mfuatiliaji wa makala zangu. Ni neema kubwa kwangu kuwa mshirika wako katika kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Neno la Mungu na maisha ya Mkristo.  Leo natamani tuongozane tena tujifunze kuhusu shuhuda. Bila shaka umewahi kusikia watu wengi, na hasa katika jamii ya Wakristo, wakizungumza kuhusu shuhuda.Wapo wanaoeleza jinsi Mungu alivyowatendea makuu na namna ushuhuda wao ulivyobadili maisha yao na kuimarisha imani yao. Wengine pia wameeleza jinsi baadhi ya shuhuda walizozisikia zilivyowafanya wawe na hofu au tahadhari katika kufanya mambo fulani. Leo natamani mimi na wewe tusafiri pamoja katika kujifunza kwa kina kuhusu shuhuda. Tutajaribu kujibu maswali muhimu kama vile: ·          Shuhuda ni nini? ·          Kwa ni...